Thursday, March 10, 2011

Siku ya Wanawake Duniani 8 march . Je, Unaielezeaje siku hii katika harakati za ukombozi wa mwanamke?

Taasisi ya mafunzo ya Jinsia na Maendeleo- GTI
 
Je, Unaielezeaje siku hii katika harakati za ukombozi wa mwanamke?
 
 MWAJUMA MKOMBOZI

Huyu ni moja ya walionufaika na harakati za ukombozi wa wanawake . Ni mwanafunzi wa darasa la sita chini ya udhamini wa SADC kwa kushirikiana na TGNP.
Na hivi ndivyo alivyosema kuhusu siku ya wanawake duniani.
Nawasihi wanafunzi wenzangu wasichana wasidanganyike

ANNA KIKWA

Ni siku nzuri ya kukumbusha serikali wajibu wake katika harakati za ukombozi wa wanawake na kuleta usawa katika Nyanja zote za Maendeleo.
Asilimia 30% ya wanawake na 70% kwa wanaume katika bunge la Tanzania bado hainifurahishi, kwani  azimio lilikuwa 50:50. “wanawake ni raia wa ulimwengu, wana haki zao na hizo haki sio mapambo hivyo basi zifanyiwe kazi.”

ASSENY MURO

Wamama twaweza. “Mtu yeyote asidharau harakati za ukombozi wa wanawake”.

MARY NSEMWA

 
Siku ya leo inanifurahisha moyoni sababu mimi ni mwanamke, ambaye nimeujaza ulimwengu katika kuleta uhai na kuchangia maendeleo ya nchi.
“Je, mgawanyo wa rasilimali una kwenda sawa na mchango wa wanawake katika jamii?”
L

Lilian Liundi

 
Baada ya miaka 100 ya harakati za ukombozi wa wanawake , Wanawake tumepata mafanikio makubwa sana hivyo ni vizuri kusherekea huku tukitafakari changamoto tulizo nazo na jinsi ya kukumbana nazo."Wanawake ni nguzo ya mpingu isiyo liwa na mchwa”
MARJORIE
 
Ni siku ya raha kwani inamuweka mwanamke katika  hali ya kuheshimika , ingawa bado kuna nachangahamoto nyingi ikiwemo kukosa ajira au malipo yenye heshima, vijijini wakulima na wafugaji hawapati msaada.
"Tusichoke kupambana kwani mabadiliko yapo yanaendelea katika kubomoa mfumo dume".

DOROTHY
 
Hakuna Taifa endelevu bila mwanamke, Mungu ana makusudi mema kumuumba mwanamke.
Najivunia kuwa mwanamke".

NDAYI

Hii siku ni kwa ajili ya wanawake wote bila kuwa sahau walioko pembezoni.
 Tuikumbushe serikali wajibu wake kuhusu mwanamke,Mwanamke aitambue siku hii kwa nafasi yake.   mwanamke tumkomboe kwa kumpa fursa ya maamuzi na kusikilizwa.”

JOYCE

Ni siku mwafaka wa kutambua umuhimu wa manamke duniani.mfano Bibi Titi Mohamed kwakumuangalia tu inatosha kugundua kuwa mwanamke ni wa thamani katika ukombozi wa jamii,nchi pamoja na ulimwengu mzima. “Jamii iamini mwanamke anaweza.”

FELISTER
 
Siku yawanawake duniani isiwe tu siku ya wanawake wenyewe na wanaume pia waitambue na  waoneshe ushirikiano katika kufanikisha harakati za kumkomboa mwanamke.

KENNY

Nafurahia  hii desturi ya kusheherekea siku ya wanawake duniani,sisi kama TGNP tunaungana na wanawake wote duniani kutafakari mafanikio na changamoto ambazo mwanamke amekumbana nazo katika hiki kipindi chote cha miaka mia moja  ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani na miaka 50  ya  uhuru wa Tanzania.

DEOGRATIUS

          Ni siku nzuri sababu wanawake wengi wamehudhuria katika kuibua changamoto ambazo     zinawakumba kila leo.Hivyo basi wanawake wazidi kusimama imara katika kutetea haki zao.

ELUKA 

Nimefurahi kusikia tukio hili la leo katika vyombo vya habari ikiwemo radio na magazeti, hii inaonesha kua jamii inatambua umuhimu wa Mwanamke. tuitafakari hii siku kwa undani zaidi.

DEMETRIA  


Siku ambayo inaadhimishwa ili kutambua mchango wa wanawake na thamani ya kazi zao katika jamii.”

EDWIN


Siku yawanawake duniani isiwe tu siku ya wanawake wenyewe na wanaume pia waitambue na  waoneshe ushirikiano katika kufanikisha harakati za kumkomboa mwanamke.

LILIAN K

 
Bado mapambano yapo “Mimi ni sehemu ya mapambano ya ukombozi wa wanawake

LYDIA

Naifurahia siku hii ya leo kwa sababu mimi ni  mwanamke kila mtu ananiangalia akisubiri  maendeleo kutoka kwangu.
“Mwanamke si tegemezi tena kwani ameamka katika ngazi ya familia hadi taifa.”

ANNA M

Siku muhimu kwetu kwani inaonesha tuliko toka, tulipo na tunapoelekea.kwakuangalia juhudi zetu pamoja na changamoto ambazo tumezipata katika hii miaka 100 ya kusheherekea siku ya wanawake duniani.

SADA

Wanawake wajifunze kutokua tegemezi,wajitume na kujikomboa.”Silaha ya kupambana na mfumo dume ni kutokua tegemezi”


TUMAINI

Tujifunze, na tueneze habari na maarifa ili kuelimisha na kusawazisha kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano


SEKELA

Ni siku ya kufurahia kwani kila kona unasikia neno mwanamke hiyo yote ni kwas ababu yeye ni wa muhimu katika swala zima la uzalishaji, utunzaji pamaoja na maendeleo kwa ujumla katika jamii
Mwanamke chakarika usilale.”
MAY

Ni siku muhimu kwa kila mwanamke kwani inamuinua pale alipokua na kumuweka mahala pakutambulika na kuonesha umuhimu wake na mchango wake mkubwa katika jamii .Wanawake tujiamini tuna uwezo mkubwa sana katika jamii,
”Wanawake ni chachu ya Maendeleo”.

CLARA 

Hakuna anayetakiwa kumkandamiza mwanamke”

REKHMA 


“Wanawake tumekomboka kwa kiasi fulani hivyo tukaze mwendo.”
 
 
 *    Toa maoni yako ili kuboresha maadhimisho ya siku hii. *